Tambua vitu ambavyo Incognito mode
inaweza kufanya na ambavyo haiwezi kufanya kulinda taarifa zako.
Je! Unajua modi ya Incognito ya Google Chrome huwa inafanya nini na data/taarifa zako wakati ukivijari kwenye mtandao kwa kutumia vifaa vyako kama simu.? Ikiwa sivyo, basi yakupasa kujikumbusha na kufikiria sana juu ya taarifa zako ukiwa unatumia mtandao hasa kwa kutumia google chrome au hata vivinjari vingine, kwa sababu inaonekana kuwa watumiaji wengine wamekuwa wakifanya shughuri za kimtandao bila kujua haswa matokeo yake yatakuwaje.
Modi ya incognito inafanya nini hasa?
Modi ya incognito inazuia tu
historia zako za kuvinjari kwenye mtandao kutokuhifadhiwa kwenye kifaa chako na
katika akaunti yako ya binafsi ya Google. Hii inajumuisha vitu ulivyokuwa
ukivitafuata kwenye mtandao, tovuti zilizotembelewa na kuki/cookie (ingawa
upakuaji na tovuti zilizowekwa alama/bookmarked bado zitajitokeza). Kimsingi,
ikiwa watu wengine wanapata nafasi ya kukitumia kifaa chako au akaunti,
hawataweza kuona kile ulichofanya ukiwa katika hali ya Incognito.
Upungufu kama huo hujitokeza pia
kwa njia za kuvinjari za kibinafsi kwenye (browser) vivinjari vingine kama
Firefox na Edge. Njia hizi hazikufanyi usiojulikana (anonymous) au kuficha
habari yako ya kibinafsi wakati unapoingia kwenye wavuti, na hazizuii Google, watoaji
wa huduma ya mtandao (ISP), waajiri, watoa matangazo mtandaoni au mtu mwingine
yeyote kuona au kukusanya data juu ya kile unachofanya. Hii imewekwa wazi kabisa
wakati unapofungua tu ukurasa mpya ambao upo kwenye hali ya incognito.
Ikiwa unataka kuhakikisha taarifa
zako/data zisihifadhiwe wala kuonekama na mtu mwingine amabaye kwa makusudi au
kwa Bahati mbaya anaweza kutumia kifaa chako au akaunti yako ya google kama
wewe, basi unashauriwa kutumia hali ya kutotambulika/incognito. Lakini ukitaka
kuhakikisha taarifa zako zinakuwa salama ukiwa unatumia mtandao, unahitaji
kufanya mengi Zaidi ya kutumia hali ya Incognito pekee.
Je ni kwa namna gani unaweza kuwa salama wakati unajivinjari mtandaoni
Kutegemea hali ya kutotambulika/incognito
za kuvinjari kibinafsi sio mpango mkakati salama sana hasa ukiwa unatumia
mtandao ambapo taarifa zako nyingi binafsi zinakuwa zinawekwa wazi, ingawa haipingiki
kuwa inasaidia kwa kiasi chake ikitumiwa kwa usahihi. Ili kuwa salama Zaidi ukiwa
unavinjari mtandaoni unashauriwa kutumia virtual private network (VPN).