Update mpya ya Google Photos


Update mpya ya Google Photos

Kama ilivyo katika program tumishi zingine kufanya mabadiliko google pia hufanya hivyo kwa lengo la kukidhi mahitaji ya watumiaji wa program zao, hii inatokana na kufanya tafiti na pia kukusanya maoni ya watumiaji ambayo mara nyingi yanafanyika kwenye program tumishi husika ambapo kila mtumiaji ana nafasi ya kutoa alama za ubora wa program yaani ku-rate program kwa kuipa nyota kadhaa na kisha kuacha maoni yaani comments.

Nini kipya katika program tumishi ya Google photos

Tarehe 29/06/2020 wameweza kutoa toleo jipya la google photo, ambalo litasaidia kutafutana kufufua kumbukumbu zako za picha, kwa kuongeza kitafutio (Search tab), sambamba na hilo wameunganisha ramani ambayo itakusaidia kujua ni wapi hasa ulipiga hiyo picha hii imerahisisha kukumbuka maeneo mbali mbali ambayo umewahi kutembelea.

Ukiachana na mwonekano mpya, pia icon ya program tumishi ya google photo imebadilishwa ili kuakisi toleo jipya. Vile vile kwa kupitia kitufe cha Makita (Library), unaweza kufuta picha zako zote yaani permanent delete, ikumbukwe kwamba mara nyingi watu huwa wanashindwa kufuta picha zao, kwa kuzipela kwenye sehem ya kuhidhia takaka yaan move to Bin, hii imekuwa ikitokea kwa sababu ya kitufe cha kufuta kabisa kuwa kimejificha. 

Lakini pia kama ilivyo kwa watuamiji wa program tumishi ya WhatsApp ambapo wamekuwa wakiweka status za matukio au vitu mbali mbali pia katika toleo hili jipya la google photo anaweza kuona mkusanyiko wa matukio/kumbukumbu/picha alizopiga siku hiyo yaani Recent highlights

Ili kuweza kupata mabadiliko hata tafadhari unweza ku-update program tumishi ya google photos kwenye kifaa chako.


           By Pazza.


    



Previous Post Next Post