Namna ya ku-scan hati (document) kwa kutumia Google Drive

Google Drive ni huduma ya wingu ya Google inayokuwezesha kuhifadhi na kusawazisha (synclonize) faili kwa ajili ya kurahisisha chelezo (backup) pamoja na namna ya kupata mafile hayo kutoka kwa vifaa anuwai, kama kompyuta yako ya mezani, simu janja, au tablet. Unaweza pia kutumia hifadhi ya Google kushirikisha watu wengine, kubadilishana taarifa lakini pia kuruhusu watu wengine kuhariri taarifa kwa wakati halisi.

Unawezaje kuwa na Hifadhi ya google.

Hifadhi ya google unaweza kuipata bila ghalama yoyote ilimradi tu una barua pepe ya Gmail. Kama unatumia vifaa kama simu zenye program endeshi ya Adroid basi mara nyingi google drive inakuja na kifaa chako.  Pia unaweza kuipakua mwenyewe kwenye duka la program yaani Playstore kama unatumia vifaa vyenye android OS, App store kwa vifaa vinavyotumia iOS vile vile unaweza kuipata kwenye Microsoft store kwa vifaa vinavyotumia windows OS.

Unaweza kufanya nini na Hifadhi ya Google?

Faida unazoweza kuzipata unapokuwa unatumia Hifadhi Google zinategemea sana jinsi unavyoitumia. Unaweza kutumia Hifadhi ya Google tu kuhifadhi na kucheleza nakala zako. Akaunti yako ya bure inakuja na 15GB ya uhifadhi wa bure, na una fursa ya kununua hifadhi zaidi kwa pesa chache kwa mwezi. Baada ya hapo unachoweza kufanya ni kupakia tu faili zako kutoka kwenye kifaa chako mfano kompyuta au simu yako na nyaraka Pamoja na taarifa zako zitakuwa salama kabisa.

Kwa ufupi kabisa unaweza kuitumia google drive kufanya yafuatayo;

  • Kutunza taarifa zako mfano, Nyaraka (Vyeti, Vitabu, Stakabadhi, Machapicho), Picha, Video n.k
  •  Kushirikisha nyaraka/taarifa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya mtandao
  • Kuhariri taarifa mtandaoni, taarifa moja inaweza kuhaririwa na mtu Zaidi ya mmoja hivyo kuepusha usumbufu wa kukutana.
  • Kuchapisha taarifa popote ulipo, wakati wowotw ilimradi una kifaa chako
  • Kufanya chelezo (Backup) ya taarifa zako.
  • Ku-scan hati/nyaraka zako kwa kutumia vifaa kama simu au tablet na kisha kuzipakia tena kwenye google drive.

Je unawezaje ku-scan hati/nyaraka zako kwa kutumia Google drive.

Kutokana na mabadiliko ya teknolojia taarifa nyingi sana ambazo ni rasmi zinapaswa kuwa zime-skaniwa. Mfano wa baadhi ya hizo taarifa ni Vyeti vya Elimu, mikataba ya kazi, Ripoti mbali mbali n.k. Kulingana mazoea watu wamekuwa wakienda kwenye stashonari ili kuweza kuskani hati mbalimbali kutumia vifaa kama scanner, lakini siku zinavyozidi kwenda mbele mambo yanabadilika na watu wanaanza kutumia zaidi program tumishi za bure ambazo zipo kwenye maduka ya programu kama vile Appstore,Playstore na Microsoft store, mfano CamScanner na hii ni kutokana na urahi na uharaka wa kuzitumia. Licha ya hivyo taasisi nyingi wamekuwa wakikataa kupokea hati/nyaraka zilizoscaniwa kwa baadhi ya hizi Apps kwa sababu taarifa zinakuwa zinaambatana na Hati miliki na App husika.

Ili kuepukana na usumbufu wote Google wakaamua kuja na njia ambayo ni rahisi na inayokubalika ambayo inaweza kutumiwa na mtu au taasisi yeyote, wakati wowote na ukiwa popote pale ilimradi tu una kifaa ambacho kina uwezo wa kuwa na Google drive.

Namna ya kutumia Google drive ku-scan.

  1. Fungua Application yako ya google drive (kama hauna pakua)
  2. Baada ya kufungua bomyeza alama ya kujumlisha iliyopo upande wa kilia kwenye kifaa chako
  3. Baada ya hapo utaona vitufe/icons sita, scan ikiwa kimojawapo
  4. Fungua kitufe kilichoandikwa scan, tayaro kwa ajili ya kupiga picha ya hati unayotaka kuscan
  5. Baada ya kupiga picha utaletewa option ya rangi(kama unata rangi ya hiyo hati kama ilivyo au unataka black&White au hautakia rangi yoyote) nashauri uchague None.
  6. Baada ya kuchagua none uta-save hati yako  
      • Andika jina la hiyo hati/doc yako
      • Kama una gmail Zaidi ya moja utachagua/kama ni moja hiyohiyo acha hivo hivo
      • Tengeneza folder unalotaka hizo taarifa zikae.






Baada ya kumaliza kuhifadhi (save) taarifa zako zitakuwa zimehifadhiwa kwenye google drive, na unaweza ukafanya hivyo mara nyingi uwezavyo mpaka utakapofikia kikomo ambacho ni 15GB. Taarifa zikishakuwa zimehifadhiwa kwenye google drive zitaendelea kuwepo humo mpaka pale utakapoamua kuzifuta, unaweza kushare nyaraka, picha n.k kutoka kwenye google drive kwa kutumia njia mbali mbali kama barua pepe n.k

By Pazza.



Previous Post Next Post