Ukweli Kuhusu Sabato

Sabato, kama tunavyoijua katika Agano Jipya, SI kushika siku fulani.  Hatuna amri yo yote ya kushika/Kuazimisha Jumamosi kuwa Sabato, wala hatuna amri yo yote ya kushika siku ya kwanza ya juma, ambayo ni Jumapili, kama Sabato.Watu wengi hushika siku.  Wengine hufanya Jumapili kuwa sanamu, siku ya ibada.  Wengine hufanya Jumamosi kuwa siku ya ibada.  Wote wanaoabudu Jumapili na washika Sabato wamekosea kabisa, kulingana na Neno la Mungu.  Sabato kwa Mkristo si kushika tena siku takatifu, mwezi mpya au majira.  Inamaanisha “pumziko la milele” kwa nafsi ya mtu kwa Kuzaliwa Upya.  Inatupasa kwenda kwa Neno la Mungu, si kwa yale Waadventista wanasema, wala kwa yale Waprotestanti husema, wala kwa yale Wakatoliki husema.

Huu hapa ukweli wa Sabato, ambayo ina maana ya “KUPUMZIKA.” 

Waebrania 4:8, “Kwa maana kama Yesu angaliwapa RAHA (au siku ya kupumzika), asingalisema baadaye juu ya siku nyingine. Basi, imesalia raha (kushika Sabato) kwa watu wa Mungu.  Katika raha yake, yeye naye amestarehe katika kazi zake mwenyewe, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake.”

Ukisoma maneno muhimu katika sehemu ya mwisho ya mstari huo, inasema kwamba “Mungu alistarehe na kazi zake mwenyewe.”  Mungu aliwapa Israeli siku ya saba kwa ajili ya Sabato yao, katika ukumbusho wa kazi yake mwenyewe ambapo aliumba ulimwengu na vyote vilivyokuwa ndani yake, kisha akaacha kuumba.  Aliacha kazi zake.  Alipumzika.  Sasa ilikuwa sawa kuwapa pumziko la Sabato watu ambao walikuwa wote mahali pamoja kwa wakati mmoja, ili wote waweze kutunza siku fulani.  Leo nusu ya ulimwengu iko kwenye nuru huku nusu nyingine iko gizani, kwa hiyo haingefanya kazi hata kidogo.  Lakini hiyo ni hoja tu kutoka kwenye maumbile ya asili.

Hebu tuone kile ambacho Biblia inatufundisha kuhusu pumziko hili la Sabato.  “Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake.”  Kuingia huku sio kuingia tu, lakini kubaki ndani, ya pumnziko.  Ni ‘pumziko la milele’ ambalo siku ya saba ni mfano tu, kwa Mkristo.

`Saba’ ukamilifu.  `Nane’ ni siku ya `kwanza’ tena.

Ufufuo wa Yesu ulikuwa katika siku ya kwanza ya juma, ukitupa uzima wa milele na pumziko la milele la Sabato.  Hivyo tunaona ni kwa nini Mungu hakuweza kutupa siku moja fulani ya juma kama Sabato (pumziko).  ‘Tumeingia’ na ‘kukaa katika’ pumziko letu, jambo ambalo Israeli hangeweza kufanya, ilikuwa ni kivuli tu cha kitu halisi ambacho tunakifurahia.  Kwa nini turudi kwenye kivuli wakati tuna kitu halisi sasa?

Jinsi tunavyopokea pumziko hili, au Sabato inayoendelea, ni kwa mwaliko wa Yesu.  Alisema katika Mathayo 11:28,29, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu;…nanyi mtapata raha.  (au kushika Sabato, si siku moja, bali uzima wa milele, Sabato) kwenye nafsi zenu.”

Haijalishi ni muda gani umekuwa ukifanya kazi chini ya mzigo wako wa dhambi, iwe ni miaka kumi, miaka thelathini au miaka hamsini, au zaidi, njoo na maisha yako ya uchovu na utapata pumziko lake (Sabato ya kweli).  Yesu atakupa pumziko.

Sasa ni pumziko gani hasa hilo ambalo Yesu atatoa?

Isaya 28:8-12 “Maana meza zote zimejaa matapiko na uchafu, hapana mahali palipo safi. Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii? Je! Ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini? Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo. La, bali kwa midomo ya watu wageni, na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa; ambao aliwaambia, Hii ndiyo raha yenu, mpeni raha yeye aliyechoka; huku ndiko kuburudika; lakini hawakutaka kusikia.”

Hapa imetabiriwa katika Isaya.  Na ikawa yapata miaka 700 baadaye kwenye Pentekoste wakati wote walipojazwa na Roho Mtakatifu kama ilivyosemwa wangekuwa.  Hii ndiyo Sabato ya kweli iliyoahidiwa.  Hivyo walipojazwa na Roho Mtakatifu waliacha kazi zao za kidunia, matendo yao ya kidunia, njia zao mbaya.  Roho Mtakatifu alitawala maisha yao.  Wakaingia katika pumnziko.  Hilo hapo pumnziko lako.  Hiyo ndiyo Sabato yako. Si siku, wala mwaka, bali ni umilele wa kujazwa na kubarikiwa katika Roho Mtakatifu. Ni wewe kuacha, na Mungu anafanya.  Ni Mungu ndani yako akipenda na kutenda mapenzi yake mema.

Loo, kwamba watu wapate kuja Kwake na kupata pumziko hilo.  Kuna kilio katika mioyo yote kwa ajili ya mapumziko hayo lakini wengi hawajui jibu.  Kwa hiyo wanajaribu kutuliza kilio hicho kwa utaratibu wa kidini wa kushika siku fulani ama kukubali kanuni za imani na mafundisho ya sharti.  Lakini wakishindwa katika hilo, wengi hujaribu kunywa pombe, ulafi, na kila jitihada za kimwili, wakifikiri kwamba kwa anasa za kilimwengu kunaweza kuwa na uradhi fulani.  Lakini katika hayo hakuna raha.  Wanavuta sigara na kunywa dawa ili kutuliza mishipa yao.  Lakini hakuna pumziko katika dawa za kidunia.  Wanamhitaji Yesu.  Wanahitaji dawa ya mbinguni, pumziko la Roho.

Kisha wengi wao huenda kanisani Jumapili.  Hiyo ni nzuri lakini hata huko hawana wazo la jinsi ya kumwendea Mungu na jinsi ya kumwabudu.  Yesu alisema kwamba ibada ya kweli ilikuwa katika Roho na kweli, Yoh 4:24.  Lakini ni aina gani ya ibada unayoweza kupata katika kanisa ambalo linamjua Mungu kidogo sana linaweka Santa Claus wakati wa Krismasi na bunny wakati wa Pasaka?  Walipata wapi hilo?  Waliipata kutoka kwa wapagani na kuifanya kuwa sehemu ya fundisho la kanisa.

Lakini mtu anapomgeukia Bwana na kujazwa na Roho Mtakatifu anaacha mambo hayo yote. Ana pumziko katika nafsi yake. Kweli anaanza kuishi, na kumpenda Mungu na kumwabudu.

Sheria ya Agano la Kale ilikuwa tu kivuli cha mambo ambayo yangekuja katika Agano Jipya.  Agano la Kale linasema, “Usizini”. Agano jipya linasema “Yeyote anayemtazama mwanamke kwa kumtamani amekwisha “zini” naye moyoni mwake.  Agano la Kale linasema, “Usiue”. Agano Jipya linasema, “Anayemchukia ndugu yake bila sababu tayari ana hatia ya kuua au kuua ndugu yake.”  Ona kwamba Agano Jipya hata linaikuza maana ya Sheria. Na hivyo ndivyo ilivyo kuhusu Sabato.  Agano la Kale husema, “itakase Siku ya Sabato”. Jipya linasema, “Njooni Kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapa Sabato (raha). Kwa maana Mimi ndimi Bwana wa Sabato.” Ikiwa Yesu Mwenyewe hakuwahi kusita kuwaponya wagonjwa siku ya Sabato na alihukumiwa na Mafarisayo kwa kufanya hivyo, inafaa tu kusema kwamba Yesu hakujishughulisha tena na kufanya utakatifu ule utunzaji wa siku fulani halisi wa siku ya Sabato. 

Yesu alikuwa anatuelekeza kwenye “Kuzaliwa Upya” kama Sabato ya kweli ya kweli au “pumziko”. Je, Yesu hakumwambia Nikodemo, “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa mbinguni.” Huku “Kuzaliwa Upya” au katika hali ya “kuzaliwa mara ya pili” sasa ndiyo Sabato halisi kwa waumini wa Kikristo wa siku hizi.

Hapa katika mistari inayofuata, tunaona Mungu akituonya kwa uthabiti tuwe na hofu, tusije tukashindwa kuingia katika hiyo Sabato (raha) ya Mungu sawa na wana wa Israeli waliomkasirisha Mungu na kuangamia jangwani WAEBRANIA 3:7-19, 4 :1-11:

Kwa hiyo, kama Roho Mtakatifu asemavyo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, kama wakati wa kukasirisha, siku ya kujaribiwa nyikani; wakati baba zenu waliponijaribu, wakanithibitisha, na kuyaona matendo yangu miaka arobaini. Kwa hiyo nalihuzunishwa na kizazi kile, nikasema, Sikuzote wamepotoka mioyoni mwao; wala hawakuzijua njia zangu.  Kwa hiyo niliapa katika ghadhabu yangu, Hawataingia katika raha yangu.

Angalieni, ndugu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.  Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo Leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.

Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, ikiwa tukishikamana kwa uthabiti na mwanzo wa uthabiti wetu hadi mwisho; Maandiko Matakatifu yasema: “Leo, ikiwa mtaisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu kama wakati wa kukasirisha.”

Maana wengine waliposikia walikasirisha, lakini si wote waliotoka Misri kwa mkono wa Musa.  Lakini alikasirishwa na nani miaka arobaini?  Si wale waliotenda dhambi, ambao mizoga yao ilianguka jangwani?  Na ni akina nani aliowaapia kwamba hawataingia katika raha yake, isipokuwa kwa wale ambao hawakuamini?  Kwa hiyo tunaona kwamba hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini.

Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.

Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha ile; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu: ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote;na hapa napo, Hawataingia rahani mwangu.

Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,

Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kutokuamini.

La, bwana, hakuna, hakuna Andiko katika Biblia, wala katika Agano Jipya, la sisi kuadhimisha Jumamosi ama Jumapili.  Lakini sababu ya sisi kushika Jumapili, ni ukumbusho wa ufufuo.

 

English (The End TimeMessage)  

Pakua Pdf

Previous Post Next Post