VPN ni nini?
VPN inasimama badala ya Virtual
Private Network. Ni kama handaki maalum kwenye wavuti linaloweza kuficha data/taarifa
zozote unazotuma au kupokea ukiwa unaperuzi mtandaoni. Hii inaweka taarifa zako
kuwa siri/faragha kutoka kwa mtoa huduma wa mtandao yaani Internet Service
Provider (ISP), watoa huduma za matangazo wanaotaka kufuatilia historia ya vitu
unavyovitazama mtandaoni vile vile watu wabaya wanaotaka kuiba taarifa zako
binafsi. VPN inaweza pia kufanya uonekane kuwa uko kwenye eneo lingine tofauti
na ulilo wakati ukiperuzi mtandaoni mfano kwa kutumia VPN unaweza kuonekana uko
Arusha wakati huo uko Lusaka.
Hapo zamani, makampuni ndiyo
yalikuwa yakitumia zaidi huduama ya VPN ili kulinda taarifa/data zao zilizopo
mtandaoni, lakini hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la huduma za VPN kwa
matumizi ya kibinafsi, kwa maana hata watu binafsi wameanza kutumia huduma ya
VPN kwa kiasi kikubwa. Mifano mizuri ni kama kuunganisha Wi-Fi za jumuiya au
kuhakikisha taarifa za kifedha zinakuwa salama kwenye wavuti.
Unaweza kutumia VPN kwenye kompyuta
yako, Tablet, Simu janja, Runinga janja, au kwenye ruta (router). Kwenye kila
mojawapo ya vifaa hivyo, kutumia VPN inaweza kukusaidia usijulikane (anonymous)
kwa kuficha eneo ulilopo muda ukiwa mtandaoni na inaongeza usalama hasa pale unapounganisha
Wi-Fi ya umma/jumuiya.
Ili kutengeneza muunganisho huu
salama, utahitaji kutumia programu tumishi kwenye kompyuta yako inayoitwa VPN
client, ambayo inaunganisha kompyuta yako na seva ya VPN katika eneo lingine.
Trafiki yote kati ya kompyuta yako na seva inakuwa iko (encrypted) imesimbwa,
kuzuia watu wengine wasione taarifa/data ambayo una-share (unashiriki).
VPN Protocol: Hii ni
teknolojia ambayo VPN hutumia kutuma na kupokea taarifa wakati huo inazuia mtu
yeyote kujua hasa taarifa hiyo ni nini. Kila VPN protocol hutumia sheria na
utaratibu tofauti kuwasiliana kati ya kompyuta yako na seva ya VPN. Baadhi
zinazingatia suala la salama zaidi, wakati zingine zinazingatia uharaka na
zingine ubora hivyo zote huwa zinakuwa na kusudi Fulani.
Seva ya VPN: Ni kompyuta kubwa
yenye nguvu iliyopo sehemu tofauti na ilipo kompyuta yako na inaunganishwa na
kopyuta yako kupitia VPN. Watumiaji wengine pia wanakuwa wameunganishwa na
kompyuta hii wakati huo huo. Unapotembelea ukurasa wa wavuti kwenye kompyuta
yako, VPN hutuma ombi kwenye seva ya VPN, halafu wavuti huona ombi kana kwamba inatoka
kwa seva badala ya kutoka kwako. Hivi ndivyo unavyoweza kujifanya uko
katika nchi nyingine au eneo lingine. Mtoa huduma ya VPN mwenye seva nyingi zaidi,
na zilizopo maeneo mengi zaidi, husaidia VPN kufanya kazi haraka kwani
unashiriki kompyuta yenye nguvu na watumiaji wengine wachache.
IP Adress:
hii ni anwani yako ya mtandaoni ya kifaa chako ambayo hutumiwa na tovuti kutuma
data/taarifa ulizoziomba. Anwani yako ya IP inaweza kujumuisha taarifa juu ya
eneo ulilopo, aina ya kifaa unachotumia, na hata maelezo kama vile kivinjari
unachotumia.
Static/Ddicated
IP: ni kama kuwa na anwani maalum ya IP kila wakati unapounganisha kupitia
VPN yako. Bila hiyo, anwani yako ya IP inaweza kubadilika kila unapoingia
mkondoni. Kuwa na aina hii ya IP inasaidia kuzuia changamoto zinazowez
kujitokeza kwa kutumia IP moja na watu wengine mfano anwani (shared) iliyoshirikiwa inaweza kufungwa
kwa sababu ya tabia mbaya ya baadhi ya watumiaji wengine.
VPN inafanyaje
kazi?
VPN inafanya
kazi ya kuziweka taarifa zako kwa mfumo wa code (encrypt) na kisha kuzificha
kwenye kitu mfano wa handaki kisha kuzisafirisha kutoka eneo moja hadi jingine.
VPN inaweza pia kukufanya uonekane kama uko kwenye eneo lingine kwa kutumia
seva ambayo iko tofauti na eneo ulilopo muda huo unatumia mtandao.
Unapotumia VPN,
kwenye kifaa chako inafanya kazi ya (ku-encrypt) kusimba shughuli zote unazouwa
unazifanya kwenye mtandao au kabla ya kutuma taarifa zako kwa njia ya mtandao. Kwa
kutumia VPN taarifa zako zitafungwa (encrypted) na zitasafirishwa kwa namna ya faragha.
Wakati kwa upande mwingine yaani taarifa zinakoenda, seva ya VPN katika eneo
tofauti itazifungua (decrypt) taarifa hizo baada ya kufika, na baada ya hapo,
seva hutuma ombi lako kwa wavuti au huduma ya utiririshaji. Once a Baada ya
maobi yako kurejeshwa, seva inazifungua (decrypt) taarifa zako ten ana kisha
kuzituma kwenye kifaa chako mfano simu au kompyuta.
Wakati seva
inatuma taarifa yako, wavuti au huduma inapoona anwani ya IP ya seva inayopokea
taarifa, kwa hivyo anwani yako ya IP inawekwa faragha. Anwani ya IP huwa inabeba
taarifa kama vile eneo la jiografia ya kompyuta yako, kwa kifupi eneo ulilopo
ukiwa unavinjari mtandaoni pia huwa na taarifa za kivinjari (brawser) gani unatumia,
Pamoja na taarifa zingine ambazo zinaweza kukutambulisha. Kwa kutumia anwani
tofauti ya IP pia huzuia wengine kujiunganisha shughuli zako za kimtandao.
Mara nyingi,
utatumia huduma ya VPN moja kwenye kila kifaa chako, lakini kuna huduma kadhaa
za VPN zinazofanya kazi kwenye router yako ya Wi-Fi. Kuweka VPN kwenye router
yako inafanya iwe rahisi kuunganisha vifaa vyote nyumbani kwako na VPN bila
programu binafsi (kwa maana kwenye kila kifaa). Hii inafaida kuu mbili: Kwanza,
inakuruhusu kuunganisha vifaa zaidi ya kimoja na kwa wakati mmoja kwani watoa
huduma za VPN kawaida huhesabu router kama kifaa kimoja. Pili, inaunganisha
Televisheni janja, vifaa vya mchezo (games), vifaa vya utiririshaji, Monita za watoto,
na kifaa chochote chenye uwezo wa kuunganishwa na Wi-Fi kwa VPN.
Ni muhimu kupata
VPN ambayo inasaidia muunganisho wa wakati mmoja ili uweze kuunganisha kompyuta
yako ndogo, Tablet, na simu yako wakati kwa wakati mmoja, badala ya kuwa na VPN
kwa kila kifaa.
Kutokana na
vyanzo mbali mbali hii ndio orodha ya VPN bora kwa waka 2020 ExpressVPN,
PrivateVPN,
NordVPN,
Windscribe,
Private Internet Access, CyberGhost,
Surfshark,
TunnelBear,
IPVanish,
ProtonVPN
Vile vile kama
unahitaji VPN ya bure unaweza kutazama moja ya hizi hapa Windscribe,
Tunnelbear,
ProtonVPN